RDC
RDC
FAQ

Questions fréquentes

Fibre inakupa Internet iliyo imara (bila kukatwa), ya ubora nzuri na spidi yenye nguvu zaidi kuliko teknolojia zingine. Inatoa pia kiasi kisicho na mwisho cha data ili kuweza bajeti yako ya Telecom bila kujali matumizi.

Kwa sababu ya spidi yake, fibre itabadilisha matumizi yenu. Munaweza tumikisha Internet mukiwa wengi, kwa spidi ya juu sana, bila kukatwa ama spidi ku punguza mbiyo yake.
Kwa hiyo wanamemba mbalimbali wa familia moja wanaweza tumiya Internet kwa limoja kupitiya vifaa mbalimbali (computer, tablet, smartphone, …) waki:

-Sukuma documents zenye kilo kubwa (picha, video za kibinafsi, …)
-Sikiliza muziki au kuangalia video kwenye Internet (streaming)
-Cheza michezo ya video kwenye Internet
-Furahishwa kutumikisha vitu vinavyo tumika na Internet (vifaa vya nyumbani, muziki …)
-Fanya kazi wakiwa nyumbani kama ginsi wangeli kuwa katika ofisi
-Soma na kufata mafundisho kwenye Internet
-Sumuliya pamoja na msaidizi wao wa sauti

Yote waki ona picha zinazo angara sana (HD) bila kupoteza spidi.

– Spidi ya juu sana (Très Haut Débit)
– Isiyo na mwisho
– Hakuna shurti yoyote
– Installation kwa bure
– Una uwezo waku panga budget yako vizuri, bila kushitukia

Fibre ni kamba ya kiyo ambayo inaruhusu kusafirisha kiasi kikubwa cha habari haraka. Teknolojia hii inasaidiya spidi kukuwa imara pia yaku aminika, ambayo haizoofike kulingana na njiya ndefu. Hii yote inahakikisha kuwepo kwa Internet nzuri sana pia spidi ya juu zaidi. Kwa sasa, hakuja kuwa teknolojia ingine iliyo nzuri zaidi kwa ajili ya usambazaji wa habari.

Ikiwa kata lako halija chaguliwa hadi sasa. Ni ya maana ujuwe ya kwamba tunafanya kazi kupanua eneo letu la kazi, kwa mengi zaidi tunakualika kufuata habari zetu kwenye reseaux sociaux. Ikiwa bado hauja jaza fomu la uchaguzi, tunakualika ufanye hivyo kupitiya www.jeveuxmafibre.cd / www.canalbox.cd
Tuta wasilia nawe kwa haraka ili kukufahamisha kuhusu eneyo zipya tulizo ongeza.

Beyi ya box pia installation ni USD 50, unazo lipa kwa mara moja unapo ji andikisha

Tunatumia vitu vyetu wenyewe (kamba na vingine), ina maanisha kwamba hatuta gusa vifaa vilivyo kutwa tayari ndani ya nyumba.

-Wasiliana nasi kwa 084 44 93 444 au kwa www.jeveuxmafibre.cd
-Kama ume chunguzwa tayari, mfanya byashara wetu atakuja nyumbani mwako ili uweze kusaini mkataba, ata chukuwa malipo ya box, piya malipo ya kwanza ya mwezi, kisha atakupa box ya Internet.
-Timu zetu za wa fundi zitawasiliana nawe kisha wanakuja fanya installation bila malipo yoyote. Unaweza sasa tumiya !

Uki taka kuji chunguza, tuna kualika:
– kuwasiliana na VAD wako (muuzishaji wa nyumbani)
– kutupigia kwa 084 44 93 444
– kujaza fomu inayokuwa kwenye www.jeveuxmafibre.cd
– Kutuma email kwa relationclientcanalboxrdc@gva.africa

Kwa niaba ya Canalbox, tunaomba msamaha. Kwa malalamiko yoyote tafazali wasiliana na timu la Huduma kwa wateja kupitiya 084 44 93 444

Kazi hii inaweza kufanyika kwa kiasi ya muda wa siku saba (7). Ila, muda huu unaweza badilika ku lingana na eneo piya shida zilizo patikana kwenye eneo hilo.

Malipo ya installation imelipwa tayari sababu inakuwa ndani ya beyi yaku nunuwa box.

Vifaa vyote vinaletwa na Canalbox, hakuna garama mpya utakayo fanya. Kazi yote ya installation ina fanyika kwa bure kabisa.

Hapana, kuwekwa kwa box kutafanyika kupitiya fundi anaye kubaliwa. Timu za Canalbox zitawasiliana nawe ili kusikilizana namna fundi wetu atakuja nyumbani mwako.

Timu za wafundi zitawasiliana na wewe mahali muta kutana. Ku nyoroshwa kwa fibre ita fanyika kutokeya mahali pa vifaa vyetu vya karibu mpaka nyumbani mwa mteja. Fundi atatafuta eneo mzuri ambapo Wifi itaweza kufunika nyumba pia ata hakikisha asi haribu uzuri wa vyumba vyako.

Mabadiliko kwa program yako ita fanyika wakati una po nunuwa program mupya kwenye eneo la ununuzi (point de vente).

Muda mfupi kabla program yako imalizike, utajulishwa kupitiya SMS. Utakuwa na uwezo:

– Ama kwenda kwenye duka Canal+ ya karibu na nyumbani mwako
– Au tumiya njia za malipo ya pesa kupitiya Mobile Money zinazo kubaliwa na wa shiriki wetu kama

Tafazali enenda kwenye duka la Canal+ kupata box mpya kwa bei ya 50 USD

Ukitaka kufata vipindi vya TV na SVOD kwenye Internet, tunapendekeza program yetu PREMIUM inayo kuwa na spidi ya 50 Mbps ambayo ina stahili kwa Haute Définition (DH) na Très Haute Définition (THD).
Hakikisha TV yako imeunganishwa na kebo ya RJ45 kwenye box lako ili iwe imara vizuri.
Kwa mwisho, chagua program moja ya kibiashara (MyCanal, Netflix, Youtube, Video ya Amazon, Apple TV, …) ambayo ina utaratibu wa uboreshaji wa bande passante kwa uzoefu bora wa TV kwenye Internet.

Ikiwa Internet yako inakuwa polepole kuliko kawaida, angalia vitu hivi :

-Hakikisha ishara yako ya WIFI iko bora. Ikiwa ni lazima, jogeya karibu na box lako
-Hakikisha hakuna vifaa vingi zaidi vinavyo tumika kwa wakati moja
-Pima usawa wa spidi yako kupitiya https://www.speedtest.net/
-Wasiliana na Huduma kwa Wateja ukiwa elezeya matokeo ya vipimo vya spidi ulivyo fanya, ikiwa haujapata suluhisho

Kuwepo kwa Wifi inategemea sana gisi nyumba ilivyojengwa, hasa kwa suala la ukubwa wa vyumba piya namna nyumba ilijengwa (béton armé, matofali, kioo, … ), pamoja na mazingira ya umeme ya mteja ambayo inaweza kuunda tatizo Fulani (Babyphone, micro-ondes, Bluetooth, …). Ufundi wa ishara ya WIFI zilizowekwa ndani ya Canalbox zina uwezo waku funika hadi 15m kwa eneyo iliyo wazi na katika mazingira yasiyo na shida fulani. Ikiwa hii haitoshi kwa ajili ya nyumba yako, chaguzi tofauti zinaweza onekana kwenye soko:

1.Tumiya teknolojia inayo itwa repeteur WIFI
2.Kuwekwa kwa teknolojia inayo itwa Courant Porteur en Ligne (CPL)
3.Kuweka vifaa vya WIFI Mesh

Enenda kumu ona muuzishaji wa vifaa vya High Tech kwa suluhisho linalolingana na mahitaji yako.

Kwa shida yoyote ya kiufundi, tafazali wasiliana na huduma kwa wateja kwenye 084 44 93 444, wataku pokeya tangu siku ya kwanza ya juma mpaka siku ya posho, tangu saa mbili asubui (7h) hadi saa mbili usiku (21h) na siku ya Mungu kutoka saa tatu asubui (9h) hadi saa nane mchana (14h).

Hatua ya 1: Nenda kwenye ukurasa ambao umeunganishwa na Internet Wifi yako, kupitia computer, tablet au smartphone, fungua njiya ya chaguo lako na uingize kwenye mustari ya anwani: https://my.canalbox.africa/login
Hatua ya 2: Ingiza nambari yako
Hii inaanza na ALCL ikifuatwa na sillabu 8 kwenye mfuniko wa box
Hatua ya 3: Chagua neno siri lako mpya
Hatua ya 4: Kubali mabadiliko.